NYATI AGONGWA NA GARI MIKUMI, ASKARI WAGAWANA NYAMA YAKE

Hivi karibuni nikiwa na usafiri wa pikipiki nikitokea Kilombero nikikatiza kwenye mbuga ya wanyama ya Mikumi na kukuta wafanyakazi wa mbug... thumbnail 1 summary
Hivi karibuni nikiwa na usafiri wa pikipiki nikitokea Kilombero nikikatiza kwenye mbuga ya wanyama ya Mikumi na kukuta wafanyakazi wa mbuga hiyo'Magemu' wakigawana minofu ya nyama ya nyati aliyegongwa na gari kwenye barabra kuu ya Morogoro-lringa iliyokatiza kwenye mbunga hiyo.

Baada ya kuwachapa picha magemu hao wakiwa bize na kazi hiyo baadae waliamua kunizawadia mguu wa nyuma wa nyati huyo,na kwamba walipohojiwa walidai kwamba nyati huyo alipojaribu kuvuka barabra hiyo aligondwa na Fusso.

Kufuatia matukio hayo ya wanyama kugongwa mara kwa mara serikali inampango wa kuihamisha barabra hiyo ambapo kigogo mmoja wa wakala wa barabra mkoa wa Morogoro'TANROARD' Alida kwamba mchkato wa kuihamisha barabra hiyo imeshafanyika kinachosubiriwa kwa sasa ni utekelezaji.

"Unajua mbali na wanyama kugongwa na magari lakini pia watu wanaotumia barabara hiyo hushuhudia wanyama bila kulipia jambo ambalo linaikosesha serikali mapato,kwa mfano ukipita majira ya jioni unaweza kuona wanyama wote akiwemo simba,tunaihamisha barabara hii na kuipitisha Dumila, Kilosa na kueleka Iringa"alisema kigogo huyo.
Danstan Shekidele